upload
The College Board
Industry: Education
Number of terms: 11179
Number of blossaries: 0
Company Profile:
The College Board is a not-for-profit membership organization that was formed in 1900 with the mission to promote excellence and equity in education through programs for K–12 and higher education institutions, and by providing students a path to college opportunities, including financial support ...
Mamlaka yaliyopewa serikali ya kitaifa na Katiba lakini yakanyimwa majimbo. mfano mmoja ni kuweka na kukusanya ushuru
Industry:Government
Mamlaka yaliyopewa kwa Seneti kukubali au kukataa majina ya walioyeuliwa na rais kuhudumu kwenye serikali au mahakama. Seneti huhitaji wingi wa kura kumwidhinisha au kumkataa aliyeteuliwa kwa mujibu wa Kipengele cha II, Sehemu ya 2, Ibara ya 2 ya Katiba. Seneti imeweza kukataa kuidhinisha watu tisa walioteuliwa kuwa Mawaziri ingawa wengi wameweza kuondolewa majina yao kwa kuhofia kukataliwa na Seneti.
Industry:Government
Mkubaliano wa watu wa nchi kuwa chini ya mamlaka ya serikali. Wanafalsafa wa haki za kibinadamu kama vile John Locke wanaamini kuwa serikali yoyote halali sharti ipate mamlaka yake kutoka kwa mwitikio wa wanaotawaliwa.
Industry:Government
Kundi la wakaazi wanaowakilishwa na afisa wa umma amaafisa yeyote aliyechaguliwa.
Industry:Government
Hali ambayo inamhitaji mtu kutoa ahadi ya kutii serikali na humfanya kustahili haki na ulinzi unaotolewa na serikali.
Industry:Government
Somo kuhusu majukumu, haki na wajibu wa serikali na uananchi.
Industry:Government
Kesi ya kisheria dhidi ya mtu au kundi la watu ili kutekeleza au kulinda haki ya kibinafsi; kuepusha dhuluma kwa mtu binafsi ama kupata fidia dshuluma kwa mtu binafsi alilofanyiwa. Hii ni tofauti na kesi ya jinai ambayo huhusisha uhalifu ama dhuluma kwa umma.
Industry:Government
Kukataa kutii sheria fulani ili kuwashawishi walio kwenye mamlaka kuzibadilisha. Uasi wa kiraia huwa na sifa ya kutumia mbinu zisizohusisha vurugu kama vile kususia kazi na kukataa kulipa kodi. Kasisi Dkt. Martin Luther King Jr.alikuwa mmoja wa Wamarekani waliounga mkono uasi wa kiraia kama njia ya kufanya sheria ziwe za kuleta haki.
Industry:Government
Mkusanyiko wa sheria ambazo huangazia haki za watu binafsi. Sheria ambazo si za kiraia ni sheria za jinai.
Industry:Government
uhuru wa kibinafsi ambao zaidi umelindwa na kipengee cha Haki za Binadamu dhidi ya kuingiliwa na serikali.
Industry:Government